Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twiga Stars yaitumia salamu Congo

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kambi ya timu ya Taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ imenoga zikiwa zimebaki siku chache kucheza mechi ya awali ya kuwania kufuzu mashindano ya Olimpiki dhidi ya DR Congo.

Twiga Stars itavaana na DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu mashindano ya Olimpiki mwakani utakaochezwa keshokutwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza jana, Kocha wa Twiga Stars, Bakari Shime alisema ana matumaini ya kushinda mchezo huo kwa kuwa ana kikosi imara cha ushindani.

“Tunajiandaa kwa mchezo muhimu dhidi ya Congo ambao ni lazima tushinde nyumbami ili kujiweka katika mazingira mazuri tutakapokuwa ugenini.

“Maandalizi yanakwenda vizuri kwa juhudi kubwa, kutokana na ari ambayo wachezaji wanayo naamini tutafanya vizuri katika mchezo huo,”alisema Shime.

Mshambuliaji Fatuma Mustapha alisema ni mchezo muhimu kushinda na amewaomba mashabiki kwenda kwa wingi uwanjani kuwashangilia. Mchezaji huyo mwenye uwezo wa kufunga ameahidi kuifungia Twiga Stars mabao matatu katika mchezo huo.

Kipa wa Twiga Stars Fatuna Omari alisema wamejiandaa vizuri kwa mchezo huo kwa kuwa wamepata mafunzo na mbinu bora za kuitungua DR Congo.



Chanzo: mwananchi.co.tz