Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tuutunze mradi wa maji Pugu-Gongo la Mboto

5388526af0e458470c42928c92fb8dda Tuutunze mradi wa maji Pugu-Gongo la Mboto

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Kuzinduliwa kwa Mradi wa maji wa Pugu-Gongo la Mboto ambao utahudumia maeneo ya Kusini mwa Dar es Salaam unadhihirisha namna ambavyo serikali ya awamu ya tano iko makini katika kutatua kero za maji nchini.

Kutokana na uzinduzi huo ulioshuhudiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu wananchi wa Jimbo la Ukonga hususani katika maeneo ya Pugu, Pugu Majohe, Gongo la Mboto, Chanika, Ukonga, Mbuyuni, Pugu Machimbo, Pugu Stesheni, Mnadani, Mongo la Ndege na maeneo mengine ya Jimbo la Segerea sasa watakuwa na uhakika wa maji.

Tunaipongeza Serikali kwa kuutekeleza mradi huu kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) kwa gharama ya Sh bilioni 6.9.

Kwa kutekelezwa kwa mradi huo ambao ni sehemu ya mipango na juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha ifikapo mwaka 2030, Watanzania wote nchini wanafikiwa na huduma ya majisafi na salama, kunazidi kupunguza pengo la asilimia la watu wasiokuwa na maji safi na salama.

Pamoja na kuipongeza serikali kwa juhudi hizi za kuwapatia wananchi majisafi na salama, tumaamini kwamba wananchi wataweza wananchi watatunza miradi hii ambayo ni mwarobaini wa magonjwa ya mlipuko yakiwemo magonjwa ya tumbo na kipindupindu.

Pia tunawapa hongera kwa sababu kukamilika kwa mradi huo kunapunguza muda kwa akina mama kutembea muda mrefu kutafuta maji, kunapunguza migogoro ya kifamilia hususani kwa wanandoa pamoja na kuokoa muda ambao wananchi watautumia katika shughuli za uzalishaji na biashara badala ya kutafuta maji.

Mafanikio yaliyopatikana katika ujenzi wa mradi huo, yanaonesha kwamba wataalamu wa Kitanzania wanweza kubuni na kutekelez amiradi mikubwa kwa gharama nafuu zaidi kuliko kutegemea ufadhili na wataalamu kutoka nje.

Tunachowaomba watendaji wetu kwa kuangalia kazi iliyofanyika katika mradi huu kuongeza ubunifu, utayari na utashi wa kuwatumikia wananchi kwa kutekeleza ilani kwa vitendo.

Kwa kuwa mradi huu tayari umeshaanza kubadilisha historia na maisha ya watu wa Jimbo la Ukonga na Segerea kwa kuondoa kilio chao cha muda mrefu, wananchi wanastahili kutambua kwamba miradi hii haikuja bure hivyo ipo muhimu wa kulinda miundombinu yake na kutoharibu vyanzo vya maji.

Hivyo sisi tunatoa wito kwa wananchi kuufanyia kazi ushauri wa serikali wa kuitunza miundombinu ya maji hiyo kwani kama wakiihujumu, watakuwa wanajihujumu na kujiumiza wenyewe.

Viongozi wa serikali za mitaa na vijiji katika maeneo yote yaliyopitiwa na mradi kushirikiana na wananchi wao kuhakikisha miundombinu ya maji inakuwa salama na kutumika kw amuda mrefu ujao ili waendelee kupata huduma bora na ya uhakika ya majisafi na salama.

Chanzo: habarileo.co.tz