Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Tunakung'uta mavumbi, Mama amesema kazi iendelee" Sabaya baada ya siku 21

WhatsApp Image 2021 04 06 At 18.55.37 660x400.jpeg "Tunakung'uta mavumbi, Mama amesema kazi iendelee" Sabaya baada ya siku 21

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

“Leo tunafikia mwisho wa maombolezo ya kitaifa yaliyotangazwa na Rais wa Nchi Mama Samia Suluhu Hassan siku ya tarehe 17 March kutokana na kifo cha shujaa wetu mwendazake JPM” DC Sabaya

“Kesho bendera zitarudi kwenye kimo chake shujaa JPM tumekuomboleza kwa siku 21, lakini nafsi zetu zitakusherehekea kwa kazi ulizofanya hadi tutakapokutana baadae!, kwa kuwa ni lazima tuamke sasa na kuishi urithi uliotuachia, tunakung’uta mavumbi rasmi na tunakoma kulia ili tusiwaumize wanaotegemea huduma zetu” DC Sabaya

“Tunaamka tena kwa faraja na hamasa ya mrithi wako anayeongoza vita kwa kutusalimu katika jina la”Jamhuri hii ya Muungano wa Tanzania, akitaka kazi iendelee” DC Sabaya

“AMESEMA” Acha dhoruba ipige, upepo uwe mwingi ila Lazima Jahazi lifike “. Endelea kupumzika kwa Amani, Huku duniani tutaendelea na kazi hadi tutakapokutana baadae kwenye pumziko la Milele” DC Sabaya ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram

Chanzo: millardayo.com