Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Tumieni mawasiliano kusaka fursa’

F63216191da609a4a6979be80a4d7930 ‘Tumieni mawasiliano kusaka fursa’

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WATANZANIA wameshauriwa kutumia mawasiliano kwa ajili ya kukuza uchumi wa Taifa kwa kuwekeza zaidi katika kutafuta masoko na fursa mbalimbali ndani na nje ya mipaka yaTanzania.

Ushauri huo ulitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, Gift Msuya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Philemon Sengati katika uzinduzi wa mnara wa mawasiliano katika kata ya Kizengi wilaya ya Uyui kijijini Isuli ambao umeratibiwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL).

Msuya alisema uwepo wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali hususani katika jijini cha Isuli ni ushahidi tosha kuwa serikali ya awamu ya tano imefanya na inaendelea kufanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu za kijamii ikiwemo mawasiliano ya simu.

Alisema mawasiliano ni muhimu sana kama kulinda usalama na kukuza uchumi wa Taifa.

Aliwasisitiza wananchi wasikubali kuona watu wachache wenye malengo yao binafsi wanaharibu uwekezaji kama huo ambao serikali imewekeza kwa nguvu nyingi kwa lengo la kuwapatia wananchi mawasiliano.

Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba aliwataka wananchi wa kijiji cha Isuli kuhakikisha miundombinu ya mnara huo wa mawasiliano na miundombinu mingine ya Shirika la Mawasiliano Tanzania, inalindwa dhidi ya wahalifu.

Chanzo: habarileo.co.tz