Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tukio la Simba kujeruhi mtu na kuua ng’ombe 10 laizindua Wizara, yaita wadau

Tukio la Simba kujeruhi mtu na kuua ng’ombe 10 laizindua Wizara, yaita wadau

Thu, 12 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Watu 96 wameripotiwa kuuawa na wanyama pori kwa kipindi cha mwaka 2018/19 nchini huku 90 wakijeruhiwa.

Akifungua warsha ya siku tatu leo Desemba 8, 2019 ya kuweka mikakati ya kuwalinda watu dhidi ya wanyamapori hatari na waaribifu, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Profesa Adolf Mkenda amesema idadi hiyo ya vifo imeongezeka kutoka vifo 39 na majeruhi 37 kwa mwaka 2015/16.

Amesema, sababu za vifo kuongezeka ni wanyamapori kuingia maeneo ya binadamu kutokana na idadi ya watu kuongezeka hivyo kuweka makazi hadi kwenye njia za kupita wanyama kama vile tembo, kupungua kwa vitendo vya ujangiri ambavyo vimewafanya wanyama wawe wajasiri kutoka na kuingia maeneo ya binadamu pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Tunalinda wanyamapori hawa ili binadamu wafaidike, kazi ya kulinda ya kwanza ni kulinda binadamu na mali zao, wanyama wanalindwa kwa ajili ya binadamu, tunapenda sana kuona binadamu wanakuwa salama,” amesema Profesa Mkenda.

Amesema Serikali inahakikisha inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha uhai wa wakazi wanaoishi jirani na hifadhi wanalindwa pamoja na mali zao.

Amesema kutokana na uharibifu na madhara yaliyoletwa na wanyama hao, serikali imetumia  Sh1.4 billioni kama kifuta machozi kwa waliokumbwa na madhara kwa mwaka 2018/19 kulinganisha na Sh900 milioni zilizotumika mwaka 2015/16.

“Kazi hii ya uhifadhi ni nzuri ila inatuletea changamoto hasa usumbufu na uharibifu unaotokana na tembo, mamba, viboko, simba, fisi ambapo ukiangalia mashamba yaliyoharibiwa na wanyama hawa takwimu zimeongezeka kutoka hekta 637 zilizoharibiwa mwaka 2015/16 kufikia hekta 13,644 hadi sasa tunavyoongea,” amesema

Mkurugenzi wa wanyamapori nchini, Dk Meurus Msuha amesema wamekutana na wadau mbalimbali wakiwemo wahifadhi ili kutoa mikakati ambayo itatoa malengo katika miaka mitano ijayo ambayo itapima nini wizara ya Maliasili na Utalii imefanya kuhakikisha wanapunguza changamoto zinazowakabili akitaja changamoto kubwa ni muingiliano wa wanyamapori kwenye makazi ya watu.

Chanzo: mwananchi.co.tz