Kufutialia tukio la mbeba mkaa kutumia pikipiki maarufu kama busta Frank Kessi (33) kudaiwa kufariki dunia kwa kupigwa risasi wameiomba serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia namna ya kushirikiana kwani biashara hiyo inawasaidia katika kuendesha maisha yao na familia zao.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu wafanyabiashara hao Ramadhan Msemakweli alisema kuwa mwenzao aliuwawa wakati wa purukushani ilipotokea kati ya askari wa maliasili na wao.
Aidha Salum Bai mwenyekiti wa Kitongoji cha Kwala anaeleza Kuwa saa sita au saba usiku alisikia milio ya risasi ambapo alfajiri alisikia gari la wagonjwa akasikia taarifa kuwa kulikuwa na operesheni kukamata mabusta na kumlazima kufika Eneo la Tukio.
Kwa upande wake Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SACP Pius Lutumo alisema kuwa mtu mmoja Frank Kessi (33) alifariki dunia huku askari polisi Koplo Ramadhan (37) mwenye namba G 7247 alijeruhiwa Katika Tukio hilo.