Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tsh. bilioni nne kukarabati barabara Temeke

Barabara Temeke.jpeg Tsh. bilioni nne kukarabati barabara Temeke

Sun, 23 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiasi cha fedha cha zaidi ya shilingi bilioni 4 kimetengwa kwa ajili ya kutatua changamoto za miundombinu ya barabara za Manispaa ya Temeke katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Paul Mhere wakati wa kikao cha mapitio ya rasimu ya bajeti ya utekelezaji wa miradi ya barabara kilichowakutanisha Wakala hiyo kwa Baraza la Madiwani la Manispaa hiyo.

Mhere amesema, kiasi hicho kimetengwa ili kuondoa changamoto za ubovu wa barabara na kwa fedha hizo barabara zitajengwa kwa viwango vya changarawe, kuchongwa na lami.

Amesema kuwa hadi sasa wameshapokea bilioni moja kati ya nne na watahakikisha wanagusa barabara za Kata zote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live