Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tsh. Bil 130/- kuchimba visima, mabwawa kunusuru mifugo

24798658ae2f5edcff61b53e1fc76f13 Tsh. Bil 130/- kuchimba visima, mabwawa kunusuru mifugo

Mon, 17 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imepanga kutumia Sh bilioni 130 kwa ajili ya kuchimba visima, kukarabati na kujenga mabwawa kabiliana na ukame uliosababisha vifo vingi vya mifugo na itaanzia na maeneo yaliyoathirika zaidi.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara alipokwenda kuwapa pole wafugaji kutokana na ng'ombe 1,874 kufa kati ya Septemba, 2020 hadi mwezi huu.

"Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan ni sikivu na inawajali wananchi, imenituma kuja kuwapa pole kwa vifo vya ng'ombe wengi kutokana na ukame kwa kukosa maji na malisho," alisema.

Ulega baada ya kushuhudia mizoga ya ng'ombe katika kijiji cha Makame, Kata ya Makame, akiwa katika mkutano ya hadhara kwenye Kijiji cha Makame na Ndede alisema serikali inawapa pole, lakini imekuja na suluhisho la kukabiliana na ukame kwa kuchimba visima na mabwawa kwa ajili ya kunywesha mifugo.

Aidha, alisema serikali itasambaza nyasi za malisho ya mifugo kwa wafugaji kuzipanda, kuvuna na kuhifadhi ili kuzitumia wakati wa ukame.

Aliwataka wafugaji Kiteto na Tanzania kwa ujumla kuacha kufuga kwa mazoea, hivyo wanatakiwa kupunguza idadi ya mifugo yao kwa kuuza ili kujenga nyumba bora, kusomesha watoto na kuboresha mifugo inayobaki na kuuza sokoni ikiwa bora.

Ulega alisema wafugaji wanatakiwa kuitikia wito wa serikali wa kuweka hereni kwenye masikio ng'ombe kwa lengo la kuweka alama ili baadae wawakatie bima ili wakifa waweze kulipwa na pia wakopesheke na taasisi za kifedha.

Mbunge wa Kiteto, Edward Ole Lekaite (CCM) alimshukuru Rais Samia kwa kutenga Sh bilioni 130 kwa ajili ya kununua mtambo mmoja wa kuchimba visima, mabwawa na malambo katika mikoa yote nchini na akaomba ikifika mkoa wa Manyara kwa sababu ya ukame.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Vayan Laizer alisema vifo hivyo vinatokana uhaba wa maji hivyo ng'ombe wanapokula majani mwituni na kukosa maji miili yao inakuwa na kinga kidogo na kushindwa kujikinga na maradhi kutokana na sumu kubaki mwilini.

Kaimu Mkurugenzi Sekta ya Afya Wilaya ya Kiteto, Dk Lunonu Sigalla wakati akitoa taarifa ya athari za ukame wilayani humo, alisema kati ya Septemba mwaka jana hadi Januari mwaka huu, ng’ombe 1,874 wamekufa kutokana na ukame na waliobaki wamedhoofika sana.

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mbaraka Batenga alisema uboreshaji wa miundombinu ya mifugo unatakiwa kwa lengo la kufungamanisha na miradi ya ujenzi wa shule shikizi zaidi ya 47 zilizojengwa katika wilaya hiyo na hivyo kuzuia kuhama hama kwa wafugaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live