Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Treni ya mizigo Dar- Arusha kuanza leo

A751c30301ba6d6fcc1b0e3a47aecbb1 Treni ya mizigo Dar- Arusha kuanza leo

Thu, 13 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TRENI ya mizigo yenye mabehewa 10 itaanza safari leo kutoka Dar es Salam kwenda Arusha. Mkurugenzi wa Uendeshaji Kampuni ya Reli Tanzania (TRC), Focus Sahani aliyasema hayo jana kwenye Kijiji cha Nambala wakati akielimisha wananchi kuhusu kuzingatia alama zinazowekwa ili kuzuia ajali na kuilinda reli.

Alisema treni hiyo ya mizigo itapita leo na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi maeneo itakayopita ili kuishangilia, kwani zaidi ya miaka 30 kulikuwa hakuna usafiri huo.

"Leo treni ya mizigo yenye mabehewa kumi itapita hapa na maeneo mengine imetoka Dar es Salam hadi kuja Arusha, hivyo ndio tunaanza kufungua fursa za kibiashara na nawasihi wananchi kuzingatia vivuko vilivyowekwa ili kuzuia ajaliā€ alisema.

Nao baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Arusha wametaka vituo viwekwe karibu karibu ili kuondoa usumbufu kwa abiria, watakapoanza kupanda gari moshi hilo.

Pia walitaka uwepo wa vivuko vya kuvukia ili kuepuka madhara yatokanayo naomba ajali. Mmoja kati ya wenyeji aliyezaliwa mwaka 1926, John Edward aliomba kituo cha zamani cha Mandela kirudishwe ili kuepuka usumbufu kwa wananchi.

Naye Jumanne Ally ambaye ni mmoja wa wakazi wa eneo hilo, aliwasihi vijana kuwa makini pale wanapoendesha pikipiki (bodaboda) kuzingatia vivuko ili kuepuka ajali, kwani baadhi ya madereva bodaboda hawapo makini wanapobeba abiria na hawachukui tahadhari.

Chanzo: habarileo.co.tz