Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Treni ya abiria yapata ajali Dodoma, 29 wajeruhiwa

63147 Ajalipic

Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Watu 29 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori na treni jijini Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Protas Katambi amesema leo asubuhi Jumanne Juni 18, 2019 kuwa ajali hiyo imetokea jana saa 5.30 usiku.

Amesema ametoa maagizo kadhaa ikiwemo kumsaka dereva wa lori ambaye inasemekana aliruka kutoka kwenye lori baada ya ajali hiyo.

Shughuli ya kuondoa mabehewa ya treni inaendelea.

Mwananchi lililopo eneo la ajali, limeshuhudia ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la tukio huku polisi waliokuwa na silaha wakiwa wameimarisha ulinzi katika tukio.

Pia, kulikuwa na abiria waliokuwa wakitoka na kuingia ndani ya treni hiyo.

Pia Soma

Katambi amesema tayari wametoa maagizo kwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuondoa mabehewa yaliyoanguka pamoja na kuwatafutia usafiri abiria hao.

"Bahati nzuri na Kamanda wa Polisi (Mkoa wa Dodoma- Gilles Muroto alikuwa hapa kwenye eneo la tukio ) kwa hiyo tuliagiza abiria wapewe ulinzi wa mali zao," amesema Katambi.

Endelea kufuatilia Mwananchi

 

Chanzo: mwananchi.co.tz