Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tope lakwamisha usafiri wa Treni ya Tazara - Kilombero

Unnamed (53) Tope lakwamisha usafiri wa Treni ya Tazara - Kilombero

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usafiri wa treni katika Reli ya Tazara umesimima kwa muda usiojulikana baada ya eneo la Kijiji cha Lumumwe wilayani Kilombero kunapopita treni hiyo kujaa tope kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Akitoa taarifa leo Jumanne Aprili 2, 2024, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Danstan Kyobya amesema changamoto hiyo imetokea jana na tayari kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya pamoja na kamati ya uokozi imeshafika eneo hilo Ili kuhakikisha hali ya usafiri inarejea kama kawaida.

"Ni kweli usafiri umesimama baada ya reli ya Tazara Kijiji cha Lumumwe kujaa tope, hata hivyo tayari wataalamu wameshafika katika eneo hilo wanaendelea na kazi.

Kyobya ameahidi kutoa taarifa kamili ikiwamo ya idadi ya abiria walioshindwa kuendelea na safari kutokana na changamoto hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live