Moshi. Mtu mmoja amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa, baada ya kuvamiwa na Tembo, wakati akiwa shambani akilinda mazao yake yasiharibiwe na wanyama hao.
Kwa zaidi ya siku tano sasa makundi ya Tembo yamevamia wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Tanzania ambapo mbali na madhara kwa binadamu, pia wameharibu nyumba na mazao.
Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro Hamis Issah akizungumza na Mwananchi leo Julai 3,2019 amesema tukio hilo lilitokea juzi Jumatatu Julai mosi, 2019 mchana ambapo tembo hao walisababisha kifo cha Hansi Edes (47) Mkazi wa Mheza kata ya Maole
Issah amesema tukio hilo lilitokea wakati mwananchi huyo akiwa shambani akichunga mazao yake yasishambuliwe na tembo ambapo kundi la wanyama hao lilimvamia na kumjeruhi kichwani hali ambayo ilisababisha kifo chake.
"Wanyama hao wametapakaa maeneo mengi ndani ya wilaya hiyo huku wakiwamo tembo wawili wakiwa wanazunguka mji wa Same. Tembo hao wawili wamezua kizazaa ndani ya wilaya hiyo na kwa sasa askari wa wanyamapori wa hifadhi ya mkomazi wanajaribu kuwarudisha ndani ya hifadhi."
Kamanda amesema mtu mmoja mwanamama ambaye amemjeruhiwa na Tembo hao, jina lake halikufahamika na kwamba alikutana na masahibu hayo, wakati akikata majani ya ng'ombe.
Pia Soma
- Kingo za barabara zawapandisha kortini watu wanne
- Mtanzania ahukumiwa kifungo cha maisha Kenya
- Wananchi wamsusia mkutano DC Same