Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tembo wanaotembea mbarali kurejeshwa hifadhini

Tembo Amkanyaga Hadi Kufa Mwongozaji Wa Watalii Afrika Kusini Tembo wanaotembea mbarali kurejeshwa hifadhini

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wamewasili Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya kwa ajili ya kuanza zoezi la kuwarejesha katika Hifadhi ya Taifa Ruaha na Pori la Akiba Mpanga - Kipengere Tembo Ili kuwanusuru wananchi kuzuriwa na mali zao kuharibika na wanyama hao.

Kikosi hicho kimewasili baada ya wiki iliyopita Mbunge wa Jimbo hilo Bahati Ndingo kusema Bungeni kwa kuiomba wizara hiyo kuchukua hatua za haraka kuwaondoa Tembo hao kwenye makazi ya watu kabla hawajaleta madhara.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila ameipokea timu hiyo na kuipongeza wizara kwa kuchukua hatua za haraka na kusema Tembo wamekuwa ni tishio kwa maisha ya wananchi na mali zao, hivyo kwa ujio wao tatizo litapungua kwa kiasi kikubwa.

Kamanda wa Uhifadhi TANAPA - Kanda ya Kusini, Steria Ndaga alimhakikishia Mkuu wa Wilaya na wananchi wa Mbarali kuwa zoezi hilo litakuwa ni shirikishi likihusisha viongozi wa Chama Tawala kuanzia ngazi ya Mkoa hadi vijiji na Serikali pia ili kuleta matokeo chanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live