Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tembo wamuua mwenye shamba

65315 Pic+tembo

Wed, 3 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Bhoke Mwita (48), mkazi wa kitongoji cha Nyaisiba kijiji cha Mbalibali Wilaya ya Serengeti ameuawa na tembo wakati akiwafukuza katika shamba lake.

Wakati mkuu wa Wilaya hiyo, Nurdin Babu akisema hajapata  taarifa za tukio hilo na kuahidi kufuatilia, ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Jeremia Gitano amesema tukio limetokea  jana Julai 2, 2019 wakati mwanamke huyo akiwafukuza tembo waliovamia shamba lake na kula mazao.

"Kundi kubwa la tembo limevamia mashamba yaliyoko pembezoni,  ili kunusuru mazao yao wananchi walishirikiana kuwafukuza kwa kupiga madebe na mabati, huyo mama alishambuliwa na tembo aliyemvamia kwa nyuma. Alijeruhiwa vibaya,” amesema Gitano.

Chanzo: mwananchi.co.tz