Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Tatu Mzuka' wachomwa moto kwa wizi Arusha

D0358c5e 0c32 49b9 87f4 E3e974827be6 'Tatu Mzuka' wachomwa moto kwa wizi Arusha

Sat, 20 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askari Polisi ambaye jina lake halikufahamika kirahisi amejikuta akihaha kujaribu kuokoa maisha ya vijana wawili maarufu 'Tatu Mzuka" wanaotumia pikipiki 'Bodaboda' zisizo na usajili kufanya matukio ya uhalifu baada ya leo kujikuta katika mikono ya raia wenye hasira kali.

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia 'Daily News Digital' kuwa vijana hao walionekana tangu jana wakifanya doria ya kutenda uhalifu na kwamba leo walipojaribu kumuibia mtembea kwa miguu wananchi waliwazingira na kuanza kuwaadhibu.

Tukio hilo limetokea katika eneo la Uzunguni ambapo raia wenye hasira waliamua kujichukulia sheria mkonono baada ya kushuhudia vijana hao wakivutana na mtembea kwa miguu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live