Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la umeme Kigamboni kuwa historia

44124 UmemepicTatizo la umeme Kigamboni kuwa historia

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Malalamiko ya wakazi wa Kigamboni kuhusu upatikanaji wa umeme yatafikia tamati Machi 6 mwaka huu baada ya kukamilika kwa kituo kidogo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini.

Kituo hicho kilichejengwa kwa ajili ya kusambaza umeme Kigamboni kinatarajiwa kuwa na megawati 20 na kinatarajiwa kuanza kazi Machi 6 mwaka huu.

Katibu mkuu wizara ya Nishati, Dk Hamis Mwinyimvua amekitembelea kituo hicho leo na kukuta wataalam wakiendelea na kazi ya kuandaa nyaya zitakazovushwa Kigamboni.

Dk Mwinyimvua ameelekeza kuwa kazi hiyo ifanyike kwa haraka ili wakazi wa Kigamboni wapate umeme wa uhakika na kwa haraka.

“Kigamboni ni eneo linalokuwa kwa kasi hivyo tuna kila sababu ya kuhakikisha tunakwenda na kasi hiyo kwa kuwapelekea umeme watumiaji wa nyumbani na hata viwandani,” amesema.

Meneja wa Tanesco Kigamboni Mhandisi Khadija Abdallah Ahmed amesema kuanza kufanya Kazi kwa kituo hicho kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko ya wakazi wa Kigamboni.

Amesema: “Yaani Kigamboni ili tuishi kwa utulivu kabisa zinahitajika megawati 50 sasa hivi tunazo megawati 17 zikiongezeka hizo 20 itakuwa hatua kubwa ikizingatiwa shughuli za viwanda huku bado hazifanyiki kwa sana.”



Chanzo: mwananchi.co.tz