Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tatizo la maji soko la Kilombero lamalizika

1065bdd48e8c4ebd04d0469298efa427 Tatizo la maji soko la Kilombero lamalizika

Mon, 9 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAFANYABIASHARA wa soko la Kilombero jijini Arusha wameondokana na tatizo la uhaba wa maji safi na salama lililodumu kwa zaidi ya miaka 10.

Kero hiyo ya uhaba wa maji sokoni hapo imetatuliwa na Taasisi ya Islamic Foundation kwa kushirikiana na Mbunge Mteule wa Jimbo la Arusha Mjini, Mrisho Gambo.

Akizindua mradi wa kisima cha maji kilichojengwa na taasisi hiyo mwishoni mwa wiki, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi alisema kisima hicho ni mkombozi kwa wafanyabishara wanaotumia maji katika shughuli zao mbalimbali hususan vyooni.

Alisema kisima hicho kina urefu wa mita 55 na kimefadhiliwa na Mbunge mteule Gambo, ambapo kimegharimu Sh milioni 20.

Alitoa rai kwa watumiaji wa kisima hicho kukitunza na kutunza miundombinu yake.

Awali, Gambo aliishukuru taasisi hiyo Kanda ya Kaskazini kwa kujitolea kuchimba kisima hicho kwa manufaa ya wananchi.

"Nawashukuru kwa moyo huu tushirikiane zaidi katika kutatua changamoto za wananchi kwani soko hili wafanyabiashara walikuwa wakilalamika kuhusu uhaba wa maji," alisema.

Mkurugenzi Msimamizi wa taasisi hiyo Kanda ya Kaskazini, Ramadhan Mfinanga alisema wametoa msaada huo kwa wafanyabishara hao ili kuwezesha kupatikana kwa huduma ya maji safi na salama.

Baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo Husna Juma na Abubakari Hussein walishukuru kupatikana kwa maji ya uhakika na kuomba changamoto ya kutozwa ushuru mkubwa itatuliwe ili waweze kuuza bidhaa zao.

Chanzo: habarileo.co.tz