Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzia: Meya wa Shinyanga Afariki Dunia

10 1?fit=640%2C464&ssl=1 Tanzia: Meya wa Shinyanga Afariki Dunia

Mon, 23 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Mathew Nkulila ambaye ni Diwani kata ya Ndembezi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu Agosti 23,2021 wakati akiendelea kupatiwa matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

Nkulila amekuwa Diwani wa kata ya Ndembezi tangu mwaka 2010 na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mwaka 2010-2015.

Nkulila alichaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Novemba 24 Mwaka 2020 na ametumikia nafasi ya Meya kwa kipindi cha miezi 10 hadi umauti ulipomkuta.

Msiba upo nyumbani kwake mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi jirani na Kanisa la Moravian, taratibu za ratiba za mazishi tutawataarifu.

Chanzo: globalpublishers.co.tz