Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kutumia Sh1.1 bilioni kufidia kaya 165 Kigongo- Busisi Mwanza

91159 Pic+fidia Tanzania kutumia Sh1.1 bilioni kufidia kaya 165 Kigongo- Busisi Mwanza

Wed, 8 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Serikali ya Tanzania itatumia zaidi Sh1.1 bilioni kuzilipa fidia kaya 165 ambazo maeneo yao yatatwaliwa kupisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi jijini Mwanza

Jiwe la msingi la ujenzi wa daraja hilo lenye urefu kilomita 3.2 linajengwa juu ya maji ya Ziwa Victoria kuunganisha Wilaya za Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza liliwekwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli Desemba 7, 2019.

Jana Jumanne Januari 7, 2020 Kaimu meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoa wa Mwanza, Pius Mwami alisema fidia hizo zimeanza kutolewa baada ya kazi ya uthamini na uhakiki wa mali na ardhi ya wananchi kukamilika.

"Malipo haya ya fidia ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Magufuli wakati wa uwekaji jiwe la msingi Desemba 7, 2019," alisema Mwami

Aliwataka wote wanaopokea fidia kuondoa mali zao ndani ya siku 30 baada ya kupokea malipo yao ili kupisha mradi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa niaba ya wananchi waliopokea fidia, Mariam Chacha na Lucas Lugomoja waliahidi kuondoa mali zao ndani ya muda wa siku 30 zilizowekwa na Serikali.

"Tunaishukuru Serikali kwa kutekeleza ahadi ya Rais Magufuli ya kuwalipa fidia wananchi wote ambao mradi utaingia kwenye maeneo yao. Nasi tunaahidi kuondoa mali zetu ndani ya muda uliowekwa," alisema Lugomoja

Utakapokamilika, daraja la Kigongo-Busisi litakuwa ndilo refu kuliko zote katika ukanda wa Afrika Mashariki huku ikishika nafasi ya sita kwa bara la Afrika.

Kwa hivi sasa, wananchi wanategemea vivuko viwili vya Mv Mwanza na Mv Misungwi kuvuka eneo hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz