Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania hatarini kuwa jangwa

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Tanzania inakabiliwa na upotevu mkubwa wa maji hivyo kutishia kuwa jangwa ifikapo mwaka 2035 kama hatua za makusudi hazitachukuliwa na Serikali na wadau.

Akizungumza leo Jumatano Julai 31, 2019 katika Jukwaa la maendeleo endelevu lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi na kufanyika jijini Dodoma, Mhaidrolojia mkuu wa Wizara ya Maji, Pamella Temu amesema kwa sasa Tanzania imebakiza hatua chache kuwa jangwa.

Amesema wakati mwaka 1962 Mtanzania mmoja alikuwa akitumia lita 7,862, mpaka mwaka 2018 matumizi yamekuwa ni lita 2,365.

“Kwa sasa Tanzania inakaribia kwenye mstari wa mwisho wa upungufu wa maji kwani hadi mwaka 2018 matumizi kwa mtu mmoja yalikuwa lita 2,365 kwa mwaka. Ifikapo mwaka 2025 matumizi yatakuwa lita 1925 kwa mwaka,” amesema Temu.

Amesema ifikapo mwaka 2035 matumizi yatakuwa lita 1,605 ambacho ni kiwango cha chini ya upatikanaji maji na mwaka 2050 matumizi yatakuwa lita 434 kiwango ambacho alisema kitakuwa ni jangwa.

Amesema wakati maji yakiendelea kupungua, mahitaji ya maji yanaendelea kuongezeka ambapo kufikia mwaka 2035, Tanzania itahitaji lita 57,560 milioni kwa mwaka sawa na asilimia 44.3.

Pia Soma

Mbali na maji, Mkurugenzi wa idara ya misitu na ufugaji nyuki wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Ezekiel Mwakalukwa ameshauri watumiaji wa maji katika kilimo, viwanda na majumbani kuchangia upotevu wa maji ili kulinda misitu.

“Mfano mwaka 2017, umeme uliozalishwa kutumia maji ulikuwa megawati 567.7 sawa na asilimia 40.54 ya jumla ya megawati 1400.34 zilizozalishwa nchini. Tanesco wanashangilia lakni hawajachangia kitu kwenye upotevu wa maji,” alisema Dk Mwakalukwa.

Mkutano huo uliofunguliwa leo Jumatano na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, umehudhuriwa pia na mawaziri akiwemo George Simbachawene (Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) na George Mkuchika (Ofisi ya Rais- Utumimishi) na baadhi ya wakuu wa mikoa na wataalamu mbalimbali.

Chanzo: mwananchi.co.tz