Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanroads watekeleza agizo la Magufuli, wahamisha ofisi zao

79552 Pic+tanroads

Fri, 11 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), umetekeleza   agizo la Rais John Magufuli aliyewataka kuhama katika jengo  walilopanga na kuhamia jengo la Serikali.

Oktoba 6, 2019  Rais Magufuli wakati akizindua barabara ya Tunduma- Sumbawanga yenye urefu wa kilomita 223.1, alitoa  siku tano kwa Tanroads kutoka katika jengo binafsi.

Ofisi za Tanroads jijini Dar es Salaam zipo katika jengo la Airtel Morocco wilayani Kinondoni.

Soma zaidi: Magufuli atoa siku tano Tanroads kuhamisha ofisi zao, zingine mwezi mmoja

Jana Alhamisi Oktoba 10, 2019 Mwananchi lilifika katika ofisi hizo na kukuta pilikapilika za hapa na pale za baadhi ya wafanyakazi wa wakipishana  kufunga mizigo.

Tanroads walipanga ghorofa ya tatu na nne, walikutwa wakihamisha vitu siku ya nne kati ya tano zilizotolewa na Rais Magufuli.

Pia Soma

Advertisement
Mwananchi lilishuhudia baadhi ya mali mbalimbali zikiwa zimefungwa kwenye maboksi tayari kupakizwa katika magari na kuhamishiwa katika jengo la Serikali.

Soma zaidi: Magufuli atoa siku tano Tanroads kuhamisha ofisi zao, zingine mwezi mmoja

Baadhi ya wafanyakazi wa taasisi hiyo hawakuwa tayari kuzungumza lolote wakidai kuwa sio wasemaji, lakini walisikika wakisema  mchakato ulianza muda mchache baada ya agizo la Rais Magufuli.

“Kwa hali inavyokwenda kesho tunaweza kumaliza mchakato wa kuhamisha vitu ambavyo vinapelekwa kwenye ofisi mpya zilizopo karibu na ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere,” alisikika mmoja wa mfanyakazi.

 Soma zaidi: Magufuli atoa siku tano Tanroads kuhamisha ofisi zao, zingine mwezi mmoja

Mfanyakazi mwingine alisikika akisema “Hali ndio kama unavyoiona hapa watu wanahamisha vitu, ofisi ile ya Mfugale (Patrick- Mtendaji mkuu wa Tanroads) watu wanaingia na kutoka. Siku za kawaida ni nadra kufanya vile.”

Chanzo: mwananchi.co.tz