Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanroads wafyeka Mahindi Tabora

Tanroads Tabora Tanroads wafyeka Mahindi Tabora

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakala wa Barabara nchini ( TANROADS) mkoa wa Tabora imeanza zoezi la kuondosha kwa kufyeka mazao yote ambayo yamelimwa na wakulima katika hifadhi za barabara.

Zoezi hilo utekelezaji wake umeanza katika maeneo ya wilaya ya Nzega na Igunga mkoani humo ambapo umefanyika ufyekaji wa mazao ikiwemo mahindi.

Meneja wa TANROADS mkoa wa Tabora Mhandisi Raphael Mlimaji, amesema hatua hiyo imefuata baada ya elimu kutolewa mara kadhaa juu ya wananchi kutotakiwa kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo katika maeneo ya hifadhi za barabara huku wengi wao wakionekana kukaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live