Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tani 4,852 za taka zinazalishwa kila kisu Dar

Sad Uchafu Tani 4,852 za taka zinazalishwa kila kisu Dar

Mon, 23 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kiasi cha taka ngumu kinachozalishwa katika Jiji na Manispaa za Mkoa wa Dar es Salaam ni wastani wa tani 4,852 kwa siku, Kati ya hizo ni tani 317 ndio zinazorejelezwa na takribani asilimia 63 ya kiasi cha taka zinazozalishwa ndicho hukusanywa nakupelekwa dampo.

Hi inamaanisha zaidi ya asilimia 20 ya taka hizo ambazo ni wastani wa tani 970,4 huishia mitaani kwenye mitaro ya maji, mito na baharini.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Hamadu Kissiwa amesema inakadiriwa asilimia 6.5 ya taka ngumu zinazozalishwa katika Jiji na Manispaa za Dar es Salaam ndizo hurejelezwa.

Kissiwa amesema haya kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na baraza hizo kwa waandishi wa habari ikiuwa na lengo la kuongeza uelewa wa athari za mazingira zinazosababishwa na taka pamoja na shughuli nyingine za binadamu,

Aina ya taka zinazorejelezwa ni plastiki, karatasi, yuma chakavu, makopo ya aluminium, kioo na taka oza

Kiasi cha taka zilizooza zinazorejelezwa katika jiji na manispaa za Dar es Salaam ni tani 8,592,04 kwa mwezi ambapo, kiasi cha tani 3,800 hurejelezwa katika Kituo cha Bonyokwa, tani 3,200 katika kituo cha Vingunguti, tani 1,500 katika kituo cha Mabwepande pamoja na vituo vingine vinayorejeleza kiasi chatani 92,04 kwa mwezi.

Je, kwa upande wako, taka unazozizalisha unazitupa wapi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live