Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga yaongoza kusalimisha silaha

Masoko Haramu Ya Silaha Ya AK 47 Yasambaa Mji Mkuu Wa Sudan Tanga yaongoza kusalimisha silaha

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeliagiza Jeshi la Polisi lianze kuwatafuta na kuwakamata wanaomiliki silaha kinyume cha sheria.

Pia Waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni ameliagiza jeshi hilo litumie taarifa ilizonazo kuwatafuta na kuwakamata wanaojihusisha kutengeneza magobore na lifanye mapitio ya sheria na kanuni ili kuona kama iko haja ya kuzifanyia marekebisho.

Masauni ametoa maagizo hayo kupitia taarifa iliyotolewa kueleza matokeo ya usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari ulioanza Septemba Mosi hadi Oktoba 31, mwaka huu.

“Kwa mujibu wa takwimu za silaha zilizosalimishwa imeonekana idadi kubwa ni magobore,” ameeleza.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa silaha 301 zilisalimishwa kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara na mikoa mitatu ya kipolisi.

Ametaja mikoa iliyosalimisha kuwa ni Tanga ambayo silaha 138, Dodoma 76, Singida 19, Morogoro 18, Mkoa wa kipolisi Rufiji 12, Pwani 10, Songwe 9, Rukwa 6, Manyara 3, Mkoa wa kipolisi Kinondoni 3, Njombe 2, Geita 1, Arusha 1, Mkoa wa kipolisi Ilala 1, Mbeya 1 na Tabora 1.

Amezitaja aina ya sila zilizokamatwa kuwa ni bastola 4, Short gun 51, Rifle 7, G3 1 na magobore 238 sambamba na risasi 262 za aina mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live