Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga Uwasa yatekeleza miradi 10 ya maji

Tangapiic Data Tanga Uwasa yatekeleza miradi 10 ya maji

Thu, 17 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa), imesema katika mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, mamlaka hiyo imetekeleza miradi 10 ya maji yenye thamani ya Sh22.221 bilioni

Miradi hiyo imelenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi pamoja na uondoshaji wa maji taka katika jijini la Tanga, Pangani na Muheza.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Uwasa, Mhandisi Geofrey Hilly jana Jumatano Machi 16, 2022 wakati alipotembelea miradi ya maji ukiwamo mradi mkubwa wa Mowe.

“Miradi tunayotekeleza ni pamoja na uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa maji Tanga awamu ya pili ambapo ujenzi wa mradi ulianza Agosti, 2021 na unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu. Mradi huu unalenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Jiji la Tanga na miji jirani ya Kasera Mkinga na Muheza.

“Mradi huo utawezesha wakazi wa Tanga 382,095 kupata maji saa 24 kwa siku kutoka wastani wa saa 21 kwa siku za sasa na mradi wa pili ni wa uboreshaji wa huduma ya majisafi Tanga kukabiliana na Uviko-19, katika mitaa ya Maweni, Pongwe, Kichangani, Neema na Mwahako kupitia fedha za miradi ya kuboresha tahadhari ya ugonjwa wa Uviko -19 mamlaka inatekeleza mradi huo wenye lengo la kusogeza huduma ya maji ili kuwafikia wakazi wa maeneo tajwa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Injinia Hilly ametaja mradi wa tatu ambao ni ujenzi wa miundombinu ya maji kuboresha upatikanaji wa maji vijiji vya Mpirani, Ndaoya, Kibafuta, Mleni na Chongoleani ambao mradi umeanza kutoa huduma katika vituo 19 vilivyounganishwa na mtandao wa maji.

Awali, Meneja ufundi wa mamlaka hiyo Mhandisi Rashidi Shaban amesema upatikanaji wa maji ni wastani wa asilimia 90 ya wakazi wote wa miji ya Tanga, Pangani na Muheza ambapo kwa jiji la Tanga maji yanapatikana kwa wastani wa asilimia 96.

Kwa upande Ofisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Devota Mayala amesema katika kuadhimisha wiki ya maji yenye kauli mbiu ‘Maji chini ya ardhi-hazina isiyoonekana kwa maendeleo endelevu’ ambapo katika kutekeleza, kauli mbiu hiyo mamlaka hiyo imepanga kuwapatia mafunzo waandishi wa habari ili kuwajengea uelewa zaidi Tanga Uwasa inavyofanya kazi zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live