Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanga-Uwasa yatakiwa kutatua changamoto

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira jijini Tanga (Tanga-Uwasa), imetakiwa kufanyia kazi changamoto ya uchafuzi wa mazingira kwenye vyanzo vya maji vilivyopo milima ya Usambara Mashariki.

Ushauri huo ulitolewa juzi na wajumbe wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) Kanda ya Kaskazini, walipoelezea mafanikio ya kazi za uhandisi nchini kwa miaka 50 tangu kuanzishwa kwake.

“Katika kusherehekea miaka 50 tangu kuundwa kwa ERB mwaka 1968, tunajipanga kuandika kitabu kitakachoorodhesha kazi zilizofanywa na wahandisi wetu, Tanga –Uwasa haitakosekana kwa kuwa imeonyesha mafanikio,” alisema Benedict Mkama ambaye ni msajili msaidizi wa ERB.

Chanzo: mwananchi.co.tz