Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanesco yawataka wananchi Arusha kuchangamkia kuunganishiwa umeme

37899 Pic+tanesco Tanesco yawataka wananchi Arusha kuchangamkia kuunganishiwa umeme

Wed, 23 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema wakazi wa jijini hapa waishio pembezoni hawana mwamko wa kutaka kuunganishiwa nishati hiyo.

Meneja wa Tanesco mkoani wa Arusha, Herini Mhina akizungumza na Mwananchi jana Jumatatu Januari 21, 2019 ofisini kwake alisema mkoa huo una zaidi ya megawati 50 lakini mwamko wa wananchi ni mdogo wa kutaka kupata umeme.

Alisema licha ya Tanesco kuendelea kuwahimiza kujitokeza kuomba kuunganishiwa huduma hiyo, hali ya kusuasua ingalipo kwa wananchi hao tofauti na maeneo ya mijini.

“Hatujui tatizo ni nini, kwa sababu hata lile punguzo lililotolewa la kulipia Sh27,000, watu hawaombi kuunganishiwa sasa tukisema labda walikuwa wakishindwa kufanya hivyo awali kutokana na gharama. Lakini wenzao wanaoishi mijini wanachangamka,” alisema Mhina.

Alisema mahitaji ya umeme mkoani humo ni megawati 75 wakati uwezo wa kituo chao cha kusambaza umeme ni megawati 120, hali inayokifanya kiwe na ziada ya megawati 50.

Alisema ili ziada hiyo itumike wanafanya jitihada za kusaka wateja wakubwa hasa wanaotaka kuwekeza katika viwanda vikubwa, vya kati na vidogo.

“Wito wetu kwa wafanyabiashara na wawekezaji, waje wawekeze kwenye mkoa wetu kwa sababu kama nilivyoeleza awali, tuna umeme wa kutosha na hauna shida ya kukatikakatika kama awali,” alisema Mhina.



Chanzo: mwananchi.co.tz