Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanesco yatangaza mgawo wa umeme Mtwara

Umeme Ni Janga La Kitaifa: Rais Tanesco yatangaza mgawo wa umeme Mtwara

Fri, 17 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Mtwara limetoa ratiba ya saa za wananchi kupata umeme baada ya baadhi ya mashine za kuzalisha umeme kupata hitilafu kuanzia Machi 15 – 25, 2023.

Akizungumza na Mwananchi ofisini kwakeleo Machi 17, 2023, meneja wa Tanesco mkoa wa Mtwara, Tawakali Rwahila amekiri kuwepo kwa mgawo huo kutokana na uzalishaji kushuka baada ya baadhi ya mashine kupata hitilafu.

“Lindi na Mtwara wanahitaji megawati 22 ambapo kwa sasa tukizalisha kwa kiwango cha juu tunafikia megawati 18.5 ambapo kwa sasa mashine namba 12 imepata hitilafu, haizalishi kwa uwezo wake, inazalisha chini ya kiwango badala ya megawati 4.3 inazalisha megawati 1.3 ikifika muda wa pick inazimwa na kufanyiwa matengenezo ambapo inaongeza uzalishaji kwa megawati 3.

“Tunazo jumla ya mashine 13 zenye uwezo tofauti ambapo zipo namba 1 na 4 zinazo zalisha megawati 2, ambapo mashine namba 5, 6, 7, 8 na 9 zinalisha megawati 1.95 wakati namba 10 na 11 zinazalisha megawati 2, 12, 13 megawati 3 hata muda huu tunavyozungumza mashine namba 2 iko nje kwa muda mrefu tangu April 2019 ambapo namba 8 ilitakiwa kubadilishwa Otoneta tangu mwaka 2020.

“Mwisho wa mwezi huu mashine namba 8 itarudi kwenye uzalishaji ili kurudisha umeme kama ilivyokuwa kawaida kupoteza mashine yenye uzalishaji wa 4.3 imepelekea uwezo kushuka hivyo kuweka muda wa kugawa umeme ili watu wapate huduma hiyo”

“Jumanne wiki hii tulizima umeme mkoa mzima kutokana na hitilafu ya mashine na 1 hivyo kwa sasa tumebaki na mashine 9 na 3,4,5,6,7,,9,10,11 na 12 ambazo zinazalisha megawati 20 ambapo ndio uwezo wa mashine ambazo ni capacity tunaacha sehemu ya kupumua ili iwe safe tunatoa megawati 16 ambapo ni pungufu kwenye mahitaji ndio maana tuna hili ni katizo la umeme sio mgao wa umeme,” amesema Rwahila.

Chanzo: Mwanaspoti