Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanesco yaikatia umeme mamlaka ya majisafi Mugumu

68419 Pic+tanesco

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) wilaya ya Serengeti limeikatia umeme Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mugumu (Muguwasa) kutokana na kushindwa kulipa deni la Sh25 milioni waliloahidi kulipa.

Kaimu fundi mkuu wa shirika hilo, Peter Mtete amesema leo Ijumaa Julai 26, 2019 wamekata umeme baada ya Muguwasa kushindwa kulipa deni hilo kama walivyoahidi Julai 24, 2019.

Amesema awali walikuwa wakidaiwa Sh29 milioni lakini wakalipa Sh4 milioni na kuahidi kuwa Julai 24, wangelipa tena.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema anafuatilia sababu za Muguwasa kutolipa deni hilo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz