Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanesco yaagizwa kutoa kipaumbele kwa wateja wakubwa Kanda ya kati

82363 Tansecopic Tanesco yaagizwa kutoa kipaumbele kwa wateja wakubwa Kanda ya kati

Fri, 1 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amelitaka Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco), kutoa  kipaumbele kwa wafanyabiashara wa viwanda katika kuwapatia umeme ili waweze kuzalisha bidhaa na kuongeza ajira kwa wananchi.

Dk Mahenge ametoa kauli hiyo leo Jumatano Oktoba 30, 2019 Jijini Dodoma kwenye mkutano baina ya Tanesco na wateja wakubwa wa umeme wa Kanda ya Kati yenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida.

Amesema kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja kucheleweshewa huduma ya umeme kwa madai kuwa hakuna bajeti ya kuwafikishia umeme.

“Naomba sana muwe karibu na wawekezaji wenye viwanda na ikibidi muwatembelee mara kwa mara ili kujua changamoto zinazowakabili kwa sababu hawa ndiyo wanaotekeleza azma ya Serikali ya uchumi wa viwanda,” amesema Dk Mahenge na kuongeza:

“Mnatakiwa muwaze nje ya boksi kwa sababu hawa wenye viwanda ndiyo wateja wakubwa kwa hiyo kama mtawapa huduma kwa wakati, wataongeza uzalishaji na nyie mtapata mapato yenu.”

Amesema Serikali ina dhamira safi ya kuwapatia wananchi wake umeme wa uhakika ndiyo maana imetekeleza mradi bwaw kubwa la kufua umeme la Julius Nyerere litakalozalisha megawati 2,115. Kwa upande wake, Meneja wa Tanesco Kanda ya Kati, Atanatius Nangali amesema mpaka sasa kanda hiyo ina wateja 276,685, kati yao wapo wateja wakubwa 74, wa Kati 250 na wadogo 276,364.

Amesema idadi hiyo ni ongezeko la wateja 41,158 katika kipindi cha mwaka mmoja, Oktoba, 2018 walikuwa wateja 235,527

Chanzo: mwananchi.co.tz