Tanga. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) linatarajia kufanya ukarabati wa njia ya nishati hiyo kutoka kituo cha Hale kuelekea Wilaya nne za mkoani Tanga.
Lengo la ukarabati huo ni kumaliza tatizo la umeme kukatika mara kwa mara.
Ukarabati huo ni kubadilisha nyaya chakavu na nguzo 940 zilizooza kutoka Hale kwenda Wilaya ya Muheza, Korogwe, Handeni na Kilindi pamoja na kukata miti.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Julai 16, 2019 na meneja wa Tanesco Mkoa wa Tanga, Julius Sabu akibainisha kuwa mradi huo utagharimu Sh1.2 bilioni na utatekelezwa kuanzia Julai hadi Septemba, 2019.
“Siyo kwamba muda wote wa ukarabati umeme utakatika, kuna wakati tutalazimika kuukata ili mafundi waweze kufanya kazi bila kikwazo,” amesema.
Mkuu wa Wilaya Handeni, Godwin Gondwe amesema taarifa hizo ni njema kwa wananchi wa kwa sababu ukatikaji wa mara kwa mara wa nishati hiyo umekuwa ukilalamikiwa kwa muda mrefu.
Pia Soma
- Bongo movie, Swahilflix kumleta Will Smith Tanzania
- Rais Magufuli asisitiza bei elekezi zao la pamba ni Sh1,200
- NEC kuanza uboreshaji wa Daftari, Kihamia atoa mwongozo
- TCU yavifungulia vyuo vilivyofungiwa kudahili