Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanesco Ruvuma wavuka lengo kuwaunganisha wateja wapya

Umeme Field Technician Ed Fundi Umeme

Wed, 7 Jul 2021 Chanzo: ippmedia.com

Hayo yalisemwa jana na Meneja wa Shirika hilo mkoa wa Ruvuma Mhandisi Florence Mwakasege wakati akiongea na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusu hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme mkoani humo.

Alisema kuwa wateja ambao wameunganishwa umeme kwa kipindi cha Julai 2020 mpaka Machi 2021 ni 7411 ukilinganisha na lengo la mwaka la kuunganisha wateja 6000 sawa na asilimia 123 ambapo wateja ambao hajaunganishwa na huduma ya umeme mpaka Aprili 2021 ni 111tu.

Alisema kuwa mkoa wa Ruvuma una mtandao mkubwa wa usambazaji wa umeme wenye mashine umba 604 na urefu wa jumla ya Kilomita 1525.40 kwa msongo wa kilovoti 33, kilomita 146.78 kwa msongo wa kilovoti 11 na kilomita 1841.16 kwa msongo wa kilovoti 0.4/0.23.

Alieleza kuwa jumla ya miradi 127 imetekelezwa kwa kipindi cha miezi 10 ambapo,  miradi ya kuboresha miundombinu ipo 38, miradi ya kuongeza miundombinu ipo 64 na miradi inayondelea ipo 25 kwa gharama ya shilingi Bilioni 345.3. Kukamilika kwa miradi hii kumeongeza idadi ya wateja kwa kuwa miundombinu imesogezwa karibu na makazi yao.

Alifafanua kuwa mradi wa umeme unaofadhiliwa na wakala wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu mzunguko wa kwanza una lengo la kuunganisha katika vijiji 161 katika wilaya zote. Vijiji vingine vyote 235 vilivyosalia kwa Mkoa wa Ruvuma vinapelekewa umeme sasa kupitia REA awamu ya Tatu mzunguko wa pili.

Kazi ya kupeleka umeme kwenye vijiji ambavyo vilikuwa havina umeme imeshaanza kupitia wakandarasi wawili kampuni za Namis Corporate na White city.

TANESCO mkoa wa Ruvuma imejipanga vizuri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanafikiwa na huduma ya umeme, alieleza Mwakasege.

Chanzo: ippmedia.com