Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamida, wachimbaji madini wafagilia bajeti

Fri, 14 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Chama cha Wanunuzi  na Wauzaji wa Madini Tanzania (Tamida) na wachimbaji wadogo wa madini ya vito Mkoa wa Arusha na Manyara wameipongeza Bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/20 kwa kuondoa kodi za mashine za kukata madini

Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa Tamida, Sammy Mollel amesema bajeti ya mwaka 2019/20 imeondoa kilio cha wachimbaji wa madini na wauzaji wa madini nchini.

Mollel alisema kuondolewa kwa kodi za mashine za kukata na kusanifu madini, kutaongeza ajira kwa vijana wengi, lakini pia kutaongeza mapato ya serikali kwani madini mengi yatasanifiwa nchini.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite One na Tanzanite Forever, Faisal Juma amesema uamuzi wa Serikali kuondoa kodi katika mashine za kukata madini ni faraja kwa sekta ya madini.

“Kuondoa kodi katika mashine za kukata madini, inamaana Watanzania wengi wataanzisha viwanda vidogo vya kusanifu madini,”amesema.

Juma pia aliipongeza bajeti hiyo kwa kuanzisha kitendo cha kusikiliza malalamiko ya wafanyabiashara wanapokuwa na malalamiko ya kodi kwani sasa kutaongeza uwazi na uwajibikaji.

Habari zinazohusiana na hii

“Kulikuwa na shida, unakadiriwa kodi hakuna sehemu ya kulalamika lakini pia hata TRA walikuwa hawawezi kushusha bila kupata muafaka sasa kutakuwa na chombo cha tatu ambacho kitamaliza migogoro,” amesema.

MWISHO.

Chanzo: mwananchi.co.tz