Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yasitisha malipo batili ya mnara wa simu

836f0170d5f68c8d683b6f407b98c690 Takukuru yasitisha malipo batili ya mnara wa simu

Sun, 4 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mkoani Dodoma imesitisha malipo batili ya mnara wa simu huku tayari mtuhumiwa mmoja akiwa amekamatwa.

Awali Taasisi hiyo ilitoa taarifa juu ya kuendelea na uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa Lyato Bihemo wa jijini Dar es Salaam kwa kosa la ubadhirifu baada ya kubaini amelipwa Sh million 58.3 na kampuni ya vodacom na HTT Infranco LTD yakiwani malipo ya kukodisha eneo la kuweka mnara.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo uchunguzi ulibaini Bihemo amelipwa fedha hizo na kampuni ya Vodacom na HTT Infranco LTD yakiwa ni malipo ya kukodisha eneo la kuweka mnara ilihali uchunguzi umebaini eneo ulipomnara huo ni msitu wa hifadhi wa Isabe uliopo Halmashauri ya Kondoa.Kutokana na hilo Kibwengo alisema fedha hizo zingepaswa kulipwa kwa serikali ya kijiji au halmashauri.

Alisema uchunguzi umeonesha kwamba mtuhumiwa huyo alifunga mkataba wa ukodishaji kuonesha eneo hilo na vodacom 2009 kwa kipindi cha miaka 10 na kujifanya mmiliki halali wa eneo hilo husika na hivyo amefanya udanganyifu akajipatia fedha hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,Sosthenes Kibwengo alisema uchunguzi unaendelea kwa walioghushi nyaraka za umiliki wa eneo la hifadhi ya msitu wa Isabe lililoko Wilaya ya Kondoa, mahali ulipo mnara wa kampuni moja ya simu na kuweza kujipatia milioni 70 kwa njia ya udanganyifu.

"Tayari tumefanikiwa kumpata mtuhumiwa mymoja ambaye anaendelea kusaidia uchunguzi lli kuwapata wenzake kwa sasa tumezuia malipo ya mnara huo ili kwa mujibu wa sheria yalipwe kwa mmiliki halali wa eneo ambaye ni halmashauri ya Wilaya ya Kondoa,"alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz