Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yaokoa zaidi ya milioni 72 Katavi

KATAVI PCCB.webp Takukuru yaokoa zaidi ya milioni 72 Katavi

Mon, 27 Apr 2020 Chanzo: --

KATIKA kipindi cha miezi mitatu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ndani ya Mkoa wa Katavi imefanikiwa kutatua changamoto mbalimbali kwa wananchi wa mkoa huo na kuokoa pesa zaidi ya Sh. milioni 72.

Akisoma taarifa ya utekelezaji ulioanzia Januari hadi Machi 2020, Mkuu wa Taasisi hiyo mkoa wa Katavi, Christopher Nakua, amesema kiasi cha Sh. 49,000,000 zimeokolewa kutoka kwenye uchunguzi wa Mikopo Umiza.

Amesema ndani ya kipindi hicho cha miezi mitatu TAKUKURU imepokea jumla ya malalamiko 32 wakati malalamiko 21 yalihusu vitendo vya rushwa,11 yalihusu makosa mengine.

Huku akitaja idara zilizoongoza kwa kulalamikiwa kuwa ni Halmashauri za Wilaya, Manispaa, Aridhi, Vyama vya Ushirikiano ( SACCOS na AMCOS)

Amesema katika suala la ukusanyaji wa mapato na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo TAKUKURU imefanikiwa kumfukuzisha kazi Askari Mgambo aliyepokea rushwa katika ukusanyaji wa mapato.

Amesema kuwa walifanikiwa kufatilia miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh. 54,000,000.00 na miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika Shule ya Sekondari Kakese,ujenzi wa Zahanati ya Kapalala.

Hata hivyo amesema katika kipindi cha kupambana na ugonjwa wa COVID 19 wanawaonya viongozi mbalimbali waliopewa dhamana ya kusimamia mapambano dhidi ya ugonjwa huo kuwaomba rushwa wananchi wasiokuwa na ndoo za kunawia mikono,na vitakasa mikono.

Taasisi hiyo imefanikiwa kuongeza ofisi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Katavi ikiwemo Wilaya ya Tanganyika na Mlele ili kuendelea kutoa huduma kwa ukaribu zaidi kwa wananchi.

Chanzo: --