Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yaokoa mamilioni yaliyochotwa na wajanja

3f4dc66be42d0528010dc3810cf77d9b Takukuru yaokoa mamilioni yaliyochotwa na wajanja

Thu, 27 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha imefanikiwa kuokoa Sh 184,807,450 za serikali na makundi mbalimbali ya wananchi, zilizoporwa na wajanja wachache.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Kaimu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, James Ruge alisema wajanja wachache waliwadhulumu wananchi fedha hizo.

Alisema Sh 99,097,450 ni fedha za wajasiriamali wa bidhaa za kilimo wa Jiji la Arusha, waliokuwa wamedhulumiwa na Kiwanda cha Kijenge Animal Product baada ya kiwanda hicho hicho kununua bidhaa kutoka kwao kushindwa kuwalipa kwa muda waliokuwa wamekubaliana.

Fedha hizo ni Sh 289,261,303 walizokuwa wakidaiwa watuhumiwa, ambapo Julai 30 mwaka huu zilirejeshwa Sh 190,163,850.

Fedha hizo Sh milioni 54,800,000 ni sehemu ya fedha ya chama cha Arusha Cooperative Union (ACU) zinaendelea kurejeshwa baada ya mali za ushirika huo kuuzwa kinyume na utaratibu na fedha kutowasilishwa kwa chama.

Alisema Sh milioni 13 ni faida ya Ngereza ole Metemi wa Kijiji cha Olkejulenderit wilayani Arumeru aliyolipwa na Kampuni ya Moerman Bruins Flowers Ltd baada ya ng'ombe wake kupotea mwaka 2011 wakiwa chini ya ulinzi wa kampuni hiyo.

Pia Sh milioni 10 ni marejesho makubwa ya mikopo na riba (mikopo umiza) iliyokuwa inatozwa na taasisi ya mikopo ya IVOJ Microcredit Company Ltd ya Jiji la Arusha, ambapo Mwalimu Devota Lyimo wa Shule ya Msingi Muriet alirejeshewa Sh milioni tatu na Mwalimu Ndaga Mwamwaja wa Shule ya Msingi Meru alirejeshewa Sh milioni sita.

Alisema Sh milioni nne ni za wananchi wa Kitongoji cha Momela kilichopo Kijiji cha Olkungwandu Kata ya Ngarenanyuki Wilayani Arumeru, waliochangishwa na kutapeliwa na Kampuni ya Ukandarasi ya Ngieco Electrical Contractors kwa ahadi ya kuunganishiwa umeme.

Alisema Sh milioni tatu ni sehemu ya mkopo wa Sh milioni 85 iliyotolewa na serikali kupitia Wizara ya Madini kwenda kwenye kampuni binafsi ya Manyara Mining Ltd, waliokiuka makubaliano ya mkataba.

Chanzo: habarileo.co.tz