Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yabaini mapungufu miradi Njombe

Takukuru Njombe (600 X 371) Takukuru yabaini mapungufu miradi Njombe

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Njombe, imebaini uwepo wa miradi Kumi na Mbili (12) ya maendeleo yenye mapungufu madogo na kutoa maelekezo ya marekebisho kwa taasisi zinazohusika.

Mkuu wa TAKUKURU wa mkoa huo Kasim Ephraim ameyataja baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa malipo ya mafundi na wazabuni wa vifaa vya ujenzi.

Ephraim amewataka wasimamizi wa miradi na wakurugenzi wa halmashauri inakotekelezwa miradi hiyo kuhakikisha wanalipa mafundi kwa wakati ili kuepusha wizi wa vifaa vya ujenzi hali itakayokwamisha miradi kukamilika kwa wakati.

Pia amesema wamebaini katika uchambuzi wa mifumo wa Halmashauri za mkoa huo hazikusanyi kwa usahihi kodi ya zuio kwa wakandarasi wa miradi inayotekelezwa hali inayotoa mwanya wa ukwepaji wa kodi kwa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA). 16h

Chanzo: www.tanzaniaweb.live