Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru yabaini madudu miradi ya maendeleo Kigoma

FEDHA WEB Takukuru yabaini madudu miradi ya maendeleo Kigoma

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa Kigoma TAKUKURU) imebaini kuwa miradi 13 yenye thamani ya Sh bilioni 16.8 inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa Kigoma ina dosari huku baadhi ya miradi ikiwa na dosari katika nyaraka za manunuzi ya vifaa vya utekelezaji wa miradi hiyo.

Hayo yamebainishwa wakati wa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu utendaji wa taasisi hiyo kwa kufuatilia miradi mbalimbali inayotekelezwa mkoani humo kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kigoma, John Mgalla akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma amesema kuwa baada ya kugundulika kwa mapungufu hayo baadhi ya taasisi ziliandikiwa barua kufanya marekebisho na tayari baadhi ya taasisi hizo zimefanya marekebisho hayo.

Hata hivyo Mgallah amesema pamoja na marekebisho hayo zipo baadhi ya taasisi ambazo kwa sasa zimeshindwa kufanya marekebisho ikiwemo kuishiwa fedha za kukamilisha miradi akiitaja shule ya sekondari Businde iliyopewa Sh milioni 470 ambapo mradi wake umeshindwa kukamilika na fedha imekwisha hivyo taarifa ya mradi huo kuwasilishwa Wizara ya Tamisemi kuombewa fedha za kukamilisha mradi. - Aida Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa Kigoma aliutaja pia mradi wa ujenzi wa Taasisi ya uhasibu Tanzania (TIA) wenye thamani ya Sh bilioni 11 ambapo ujenzi wake unasuasua kwa mfadhili kuchelewa kutoa fedha sambamba na Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kuchelewa kutoa kibali cha kufanyika kwa tathmini ya mazingira hivyo kuchelewesha mradi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live