Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala, Tanzania umefanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh38 bilioni na kubaini upungufu katika utoaji wa malipo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 2, 2019 Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Ilala, Christopher Myava amesema katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2019 walifanya ukaguzi na uchunguzi wa tuhumiwa mbalimbali.
"Lengo la kufuatilia miradi ya maendeleo ni kuangalia thamani halisi ya fedha za umma kwenye ujenzi wa miradi ili kudhibiti uvujaji wa fedha za umma kwenye miradi ya maendeleo," amesema Myava
Amesema katika ufuatiliaji wa miradi miwili iliyoko katika sekta ya ujenzi wa barabara zilizoko maeneo yasiyopimwa katika kata ya kiwalani, ilibainika kulikuwa na upungufu katika utoaji wa malipo.
"Baadhi ya kazi za uwekaji wa zege la lami, zililipwa tofauti na ilivyoidhinishwa katika mkataba ambapo ilibainika mkandarasi alilipwa takribani Sh1 bilioni zaidi ya fedha zilizotakiwa alipwe" amesema
"Kuna barabara nyingine zilionekana kuwa na urefu mfupi tofauti na ilivyokuwa kwenye mkataba."
Pia Soma
- Mwili wa Bob Collymore kuchomwa leo
- Mwili wa mzamiaji wa ndege kutoka Kenya waanguka ikitua London
- Askofu Kasala akitaka chuo cha Saut kujitathimini