aasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo imeokoa shilingi Bilioni tatu ambayo ni kodi ya zuio baada ya kusajili taasisi 956 za Serikali zilizopo kwenye halmashauri 11 za mkoa wa Tanga zinazofanya malipo mbalimbali kwa watoa huduma na wauzaji wa bidhaa.
aasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani humo imeokoa shilingi Bilioni tatu ambayo ni kodi ya zuio baada ya kusajili taasisi 956 za Serikali zilizopo kwenye halmashauri 11 za mkoa wa Tanga zinazofanya malipo mbalimbali kwa watoa huduma na wauzaji wa bidhaa. Taarifa hiyo imetolewa kwa Waandishi wa Habari jijini Tanga na Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa huo Victor Swella ambaye pamoja na mambo mengine ameeleza kubaini uwepo wa mapungufu kwenye miradi 14 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni tano.