Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru, Polisi waagizwa kuwashughulikia watakaotorosha vyandarua

Vyandarua Rungwe.png Takukuru, Polisi waagizwa kuwashughulikia watakaotorosha vyandarua

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, Jaffar Haniu ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Jeshi la Polisi wilayani humo kuanza ufuatiliaji wa zoezi la ugawaji wa vyandarua mashuleni ili kubaini wanaotorosha na kuwachukulia hatua.

Haniu amesema leo Jumatano Novemba Mosi, Mwaka huu wakati akizungumza na Mwananchi Digital baada ya kupokea vyandarua 43,149 vilivyotolewa na Wizara ya Afya Ofisi ya Tamisemi na kuratibiwa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD).

“Wizara ya Afya imetoa vyandarua kwa ajili ya wanafunzi kujikinga na ugonjwa wa maralia sasa isitokee mtu anafanya udanganyifu wa kutorosha kusikojulikana lazima wakamatwe na kuchukuliwa hatua,”amesema.

Zoezi hilo la makabidhiano limefanyika katika Shule ya Msingi Tukuyu wilayani humo huku akisisitiza wazazi kuwasimamia watoto kulala kwenye vyandarua vyenye dawa

Aidha Mkuu huyo amesema Serikali imegawa bure kwa wanafunzi na haitapendeza wazazi kutumia kinyume na utaratibu ikiwemo kuvulia samaki na wigo wa bustani dhidi ya ndege na wanyama wengine.

“Pia nitoe angalizo na onyo kwa watu wanao potosha jamii kuwa vyandarua vina madhara kitendo hicho kinarudisha nyuma juhudi za Serikali dhidi ya mapambano wa ugonjwa hatari wa maralia kwa watoto kuanzia mwaka 0 na kuendelea,”amesema.

Mfamasia kutoka Bohari Kuu ya Dawa, Caroline Cornelius amesema zoezi la ugawaji wa vyandarua lilizinduliwa katika Mkoa wa Mbeya ambapo kwa Wilaya ya Rungwe watagawa 43,149 kwa Shule 150 zitanufaika na mpango.

Caroline amewataka walimu wakuu, kamati za Shule na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji, kutoa ushirikiano ili kukamilisha zoezi hilo katika maeneo yote yaliyoelezwa lengo ni kuona watoto wetu wanapata elimu bora na kuwa salama dhidi ya ugonjwa wa maralia.

Mkazi wa Katumba Michael, Athon amesema kuwa Serikali ina mipango mzuri changamoto ni jamii yenyewe kutokuwa na uelewa wa umuhimu wa kulala kwenye chandarua chenye dawa.

“Tunashukuru Serikali ya awali ya sita kwa kutoa bure vyandarua lakini tungeomba elimu itolewe ya kutosha sambamba na kutunga sheria za kuwabana wananchi ambao wanatumia kuvulia samaki,kutunzia bustani na mapazia kwenye milango ya vyoo,”amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live