Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takukuru Lindi yaokoa zaidi ya Sh26 millioni

Pesa Fedhaddd Takukuru Lindi yaokoa zaidi ya Sh26 millioni

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: Mwananchi

Lindi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Lindi imeokoa zaidi ya Sh26 milioni katika ufuatiliaji wa zao la ufuta kwa kipindi cha Julai na Septemba 2023.

Fedha hizo zimetokana na ufuatiliaji wa zao la ufuta la kilogramu 7001 zilizouzwa kupitia Chama cha Msingi cha Ushirika cha Mbwemkuru kilichopo Wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Akizungumza jana Ijumaa Octoba 27,2023, Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Emma Mwasyoge amesema pesa hizo zilikuwa malipo ya wakulima wa ufuta ambazo walitakiwa kulipwa msimu wa 2022/23 huku viongozi, makarani pamoja na wajumbe wa chama cha Msingi Mbemkuru wakitajwa chanzo kupotea fedha hizo.

Mwasyoge amesema viongozi hao walihusika katika kukusanya, kupina na kusafirisha zao hilo kwenda chama kikuu cha Ushirika Runali.

Amesema kiasi cha Sh5.9 milioni kiliokolewa kutoka kwa viongozi hao kimelipwa kwa baadhi ya wakulima ambao hawakulipwa fedha za mauzo ya ufuta.

"Fedha hizo zimelipa kwa wakulima chini ya usimamizi wa Ofisi ya Ushirika Wilaya ya Liwale na kiasi kilichobakia kinaendelea kurejeshwa kupitia akaunti ya chama hicho cha Msingi cha Mbwemkuru," amesema Mwasyoge.

Pia Mwasyoge amesema wanaendelea na uchunguzi wa kubaini waliohusika na ubadhilifu huo watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria, huku wakiendelea kutoa elimu ili kwa msimu wa korosho wa 2023/24 ilikouzia yaliyojitokeza kwenye ufuta.

Chama Mbemberu kimekuwa miongoni mwa chama sugu cha Ushirika ambacho kimekuwa na viongozi ambao sio waaminifu katika utendaji kazi.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainabu Telack alimuagiza Kaimu Mrajisi wa vyama vya Ushirika, Cesilia Sositenes kukifunga chama hicho kutokana na ubadhilifu wa fedha kwa wakulima.

Ayubu Bakari mkulina wa ufuta Wilaya ya Liwale ameishukuru Takukuru kwa kazi kubwa waliofanya ya kuhakikisha fedha za wakulima zimerudi.

"Kazi ya kulima ni ngumu unalima halafu wajanja wanadhulumu haki yako inauma hivyo tunaishikuru Serikali na Takukuru kuhakikisha wakulima wanapata haki yao,"amesema Ayubu.

Mwanahamis Jumbe, amesema kuwa viongozi waliokutwa na ubadhilifu huo wapelekwe mahakamani.

"Kazi kubwa wanayofanya kwa ajili yetu sisi wakulima na wananchi wanyonge, kitendo cha kurudisha fedha ni ujasiri, wakulima walishakata tamaa na pesa zao, baadhi ya viongozi kwenye Amcos zetu, wamekuwa ni watu wakujinufaisha," amesema Mwanahamis.

Chanzo: Mwananchi