Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Takataka zageuka dili Geita

Mji Wa Geita Takataka zageuka dili Geita

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Halmashauri ya Mji wa Geita mkoani hapa imeanza kutekeleza mradi wa maboresho ya ukusanyaji, uhifadhi na uchakataji wa taka, ili kuimarisha usafi wa mazingira na kuongeza mapato kupitia taka.

Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Taka na Usafi wa Mazingira Halmashauri ya Mji wa Geita, Aloys Mutayuga ameeleza hayo leo katika mahojiano maalum nasi.

Amesema hatua hiyo imeanza kwa kusambaza makontena matano ya kuhifadhi taka kwa kila kituo, kwenye vituo 10 mjini Geita ili kutoa fursa kwa watupa taka kutenganisha taka na kurahisha uchakataji.

“Tumeanza na makotena 50, na hizo kontena 50 kila moja kuanzia kuisafirisha na kuiweka hapo ilipo imegharimu shilingi milioni 1.7, kwa hiyo hizo kontena 50 zimegharimu jumla ya Shilingi milioni 85.

“Tunayaweka kando ya barabara kwa sababu kuna watu wanatembea wanakula, wanakunywa maji, wanabeba taka tofauti wanatupa kwenye mtaro, sasa hivi tunataka kudhibiti utupaji taka hovyo,” amesema.

Ameeleza utenganishaji wa taka utafanikisha mradi wa halmashauri wa taka kuzifanyia urejeshaji (recycling) kwa kuzalisha mbolea kutoka taka ozo, kuzalisha mkaa kwa makaratasi na taka za plastiki zitauzwa viwandani.

Amesema hadi sasa halmashauri ina uwezo wa kukusanya tani 2800 kati ya tani 5700 za taka inayozalishwa kwa mwezi sawa na ufanisi wa asilimia 49, huku lengo ni kufikia ufanisi wa asilimia 60 mwaka wa fedha 2023/24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live