Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taharuki! Ng’ombe wakumbwa na ugonjwa wa ajabu

Ngombe Jkg Taharuki! Ng’ombe wakumbwa na ugonjwa wa ajabu

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ugonjwa wa miguu na midomo kwa ng’ombe umezikumba kata sita za Halmashauri ya Wilaya ya Geita na kusababisha mifugo hiyo kudhoofika na kufa.

Wakizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani wa kata hizo, wamedai ugonjwa huo unasababisha ng’ombe kutokwa mate mdomoni na kushindwa kutembea lakini hata wanapowachinja, wamebaini mapafu yanakuwa yameoza.

Bila kutaja idadi ya ng’ombe waliokufa hadi sasa diwani wa Kata ya Bujura, Amina Kanijo amesema hali ni mbaya na wafugaji wanapata hasara kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo na kuomba wataalamu kufika kwenye maeneo yao ili kunusuru mifugo iliyobakia.

“Ngombe anaumwa mdomo unatoa udenda na miguu hawezi kutembea. Pia anakohoa hata ukimchinja unakuta mapafu yameoza. Ni ng’ombe wengi wamekufa na wananchi wanapata hasara, naomba mkawaelimishe ili hizi ng’ombe ambazo hazijakumbwa na ugonjwa tuweze kuziokoa,”amesema Kanijo.

Kaimu Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Hamashauri hiyo, Israel Tarimo amekiri ng’ombe kuugua na kusema tayari wamewasiliana na wataalamu wengine ngazi ya kanda kuona namna ya kunusuru na kukinga wengine wasiambukizwe.

Mwenyekiti wa baraza hilo Charles Kazungu ametaja kata ambazo tayari ng’ombe wameshambuliwa kuwa ni Kata ya Bujura, Magenge, Kaseme, Kagu, Isulabutundwe na Nyakagomba na kuwataka wataalamu kufanya juhudi za makusudi kunusuru mifugo hiyo.

“Rai yangu wataalamu chukueni jitihada za haraka kunusuru mifugo kwa kuwa mifugo hii ndio tegemeo la wananchi ingieni kazini sio muagize waliko kwenye kata nendeni katoeni elimu ya namna bora wanayoweza kunusuru mifugo yao na huu ugonjwa,”alisema Kazungu.

Halmashauri ya Geita inakata 37 na ina ng’ombe zaidi ya 163,000

Chanzo: www.tanzaniaweb.live