Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taharuki: Mbuzi 17 wakutwa wameuawa

Mbuzi Dead Taharuki: Mbuzi 17 wakutwa wameuawa

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mbuzi 17 wamekutwa katika pori lililopo mtaa wa Bombambili Halmashauri ya mji wa Geita wakiwa wamekufa huku chanzo cha mbuzi hao kufa kikiwa hakijafahamika.

Wakizungumza nasi mashuhuda waliofika katika eneo hilo wamesema licha ya taarifa hizo kusambaa kwa watu wengi mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyejitokeza kuwa ndiye mmiliki wa mbuzi hao.

“Nilipofika pale nikafikiri mbuzi hao ni wakwangu lakini nilivyochunguza hawakuwa wakwangu baada ya hapo nikampigia mwenyekiti wa mtaa ili aje kuona tukio hilo kwaiyo alifika pamoja na polisi jamii wakawa wanauliza mbuzi hawa ni wanani lakini mpaka sasa hatujui mbuzi hawa ni wanani” Maneno Lusota Kanyeti amesema Mkazi wa Bombambili

“Nilifika hapa asubuhi maana nilipewa taarifa kuwa kuna mbuzi zimekufa basi nilifika nikaona ila hatujajua nini kimesababisha mbuzi hawa wafe maana hazina hata damu kusema zimechinjwa wala nini labda tumekuta zimekufa arafu zimeachanishwa achanishwa” Teddy Mihayo amesema Mkazi wa Bombambili

“Inaonekana mbuzi hizi zimebebwa zikawekwa maana kama pengine tuseme zimekula mazao ya watu zisinge kuwa huku porini zimekufa zikiwa sehemu moja hivi arafu mafungumafungu,” amesems Meshaki Julius, Mkazi wa Bombambili

Aidha wakazi wa mtaa huo wameliomba jeshi la polisi kwa kushirikiana na wataalamu wa mifugo kufanya uchunguzi ili kujua sababu ya mbuzi hao kufa ili kuondoa wasiwasi kwa wakazi wa mtaa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live