Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taharuki! Fisi Atafuna Mbuzi 17

Fisi 2?fit=600%2C400&ssl=1 Taharuki! Fisi Atafuna Mbuzi 17

Thu, 20 May 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

WAKAZI wa Kata ya Lubaga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mkoani Shinyanga wameiomba serikali kuwasaidia kutatua changamoto ya uwepo wa wanyama aina ya fisi kwenye maeneo yao baada ya fisi hao kuvamia zizi na kuua mbuzi 17 na kondoo katika familia ya Monica Paul mkazi wa mtaa wa Azimio kata ya Lubaga.



Ndugu wa familia ya Monica Paul wamesema kuwa ilikuwa majira ya saa kumi usiku wa kuamkia Jumatano Mei 19,2021 ndipo waliposikia mlio wa fisi hali iliyo walazimu kutoka nje na baada ya kutoka nje ndipo walipogundua kuwa mbuzi wa wameliwa na fisi hao.



Wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa kwa sasa fisi hao wamekuwa wakionekana mara kwa mara katika maeneo yao tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma.



Diwani wa kata ya Lubaga Reuben Dotto ameeleza kuwa changamoto ya uwepo wa fisi kwenye maeneo yao imesababisha hofu kwa wananchi na kusababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kuhudhuria shuleni mapema wakihofia kuumwa na fisi.



Afisa mifugo wa kata ya Lubaga Eliaremisa Mbise amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuagiza wakazi wa kata hiyo kuteketeza kwa moto masalia ya mbuzi waliouawa na fisi ili kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kula mbuzi walioliwa na fisi.
Chanzo: globalpublishers.co.tz