Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Taha yaagizwa kuwezesha kutambua udongo

5d6da56a2a7676156eef52f73df43c80 Taha yaagizwa kuwezesha kutambua udongo

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya ameitaka Taasisi ya Kuendeleza Mazao ya Bustani (Taha) kuendelea kuelimisha wakulima wengi zaidi kuzingatia kilimo cha kitaalamu kwa kutambua aina ya udongo unaofaa kwa zao husika na mbolea gani itumike.

Alisema hayo alipokutana na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Dk Jacquline Mkindi, jijini Arusha kujadili mikakati na mambo yanayohusu maendeleo ya tasnia ya mboga, matunda na maua nchini.

Sambamba na kikao hicho, Katibu Mkuu Kusaya alikabidhi zawadi ya ramani ya Tanzania inayoonesha viwango vya afya ya udongo imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa Taha, Dk Jacqueline Mkindi.

Katika mazungumzo hayo, Kusaya ameitaka kuwezesha utambuzi wa maeneo yanayofaa kwa mazao ya mboga, maua na matunda nchini.

Alisema wakulima wakitambua aina ya udongo watafahamu nini kinastahili kulimwa eneo hilo hivyo kuwaongezea tija.

Sekta ya kilimo cha mboga, matunda na maua nchini imekuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji maendeleo kwa kuliingizia taifa Dola za Marekani milioni 500 kwa mwaka.

Ukuaji wa sekta hiyo umekuwa chachu ya kuvutia wawekezaji katika sekta nyingine za maendeleo nchini.

Dk Mkindi alishukuru juhudi za serikali katika kuhakikisha kilimo hicho kinakuwa na tija kwa wakulima na taifa kwa jumla

"Tunaendelea kuishukuru serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ushirikiano mkubwa na wa muda wote inaotupatia wadau wa sekta ya horticulture," alisema Dk Mkindi.

Kusaya alikuwa Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kutembelea taasisi zinazojihusisha na kilimo vikiwemo viwanda vya kuzalisha mbolea kwa matumizi ya kilimo.

Chanzo: habarileo.co.tz