Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora yaanza kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii

Tabora Yaanza Kampeni Ya Kutangaza Vivutio Vya Utalii Tabora yaanza kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii

Mon, 27 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali katika mkoa wa Tabora kupitia wilaya ya Tabora imeungana na balozi wa utalii nchini Nangasu Warema kuanza kunadi vivutio vya utalii vilivyopo katika wilaya ya Tabora na mkoa kwa ujumla kupitia kampeni inayokwenda kwa jina la talii na Mama Samia ambayo inaendeshwa na balozi huyo kwa lengo la kuunga mkono serikali katika juhudi ya kuendelea kutangaza vivutio vya utalii wa ndani ya Taifa la Tanzania kupitia mikoa mbali mbali hapa nchini.

Kampeni hiyo ambayo kwa sasa imefikishwa katika mkoa wa Tabora yenye kauli mbiu ya utalii ni uchumi inalenga kuyafikia na kuyatangaza maeneo yote ya kiutalii katika mkoa wa Tabora na hatua hiyo ni kutokana na mkoa huo kusahaulika katika eneo la kiutalii hali ambayo inalipunguzia taifa wigo wa kuingiza fedha za kigeni.

Hata hivyo wakati balozi huyo wa utalii akizungumza na wadau wa utalii na uwekezaji katika mkoa wa Tabora afisa wa Maliasili katika Manispaa ya Tabora Seif Salum ametaja zaidi ya maeneo matano muhimu yenye sifa za kiutalii ikiwemo bustani za wanyama ,makumbusho ya mali kale za kihistoria ambayo yapo katika mkoa wa Tabora .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live