Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora wadaiwa bilioni 3.1/za kodi ya ardhi, pango

6d989d5c1f26cb6f513d11b95bf07755.jpeg Tabora wadaiwa bilioni 3.1/za kodi ya ardhi, pango

Sat, 12 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI za serikali na watu binafsi mkoani Tabora wanadaiwa Sh bilioni 3.1 ya kodi ya ardhi na kodi ya pango la ardhi kwa miaka 5 sasa.

Ofisa Mipango Mwandamizi na Mratibu wa Kodi Kanda ya Kati, Tatu Simba akizungumza katika mkutano wa hadhara kata ya Isevya, Manispaa ya Tabora jana alisema kwamba kumekuwepo na malimbikizo ya ya madeni ya kodi ya ardhi na pango katika kipindi cha kuanzia mwaka 2017 hadi 2021.

“Hali hiyo inachangia kuzorotesha kwa pato la nchi ambalo ni msingi wa maendeleo na ustawi wa watanzania na kuchelewesha maendeleo ya nchi,”alisema Tatu.

Ofisa huyo alizitaka taasisi binafsi zenye madeni sugu kulipa madeni yao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa ili kufanikisha malengo endelevu ya nchi.

Akitoa ufafanuzi huo mratibu wa kodi mkoa wa Tabora, Evody Krety alisema kodi ya ardhi ni tofauti na kodi ya pango la nyumba anakuongeza kuwa kodi ya ardhi linalipwa kwa ajili ya umiliki wa ardhi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz