Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tabora kutoa Ths. milioni 852 mikopo ya wanawake, vijana wenye ulemavu

Fedha Wagawana Tabora kutoa Sh852.6 milioni mikopo ya wanawake, vijana wenye ulemavu

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, imepokea maombi ya vikundi 117 ikihitaji kupatiwa mikopo ya Sh852.6 milioni inayotolewa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Vikundi vya wanawake ndio vinaongoza vikiwa 88 kwa kuomba Sh679.6 milioni, huku vijana wakiwa na vikundi 20 vilivyoomba Sh154.9 milioni na watu wenye ulemavu vikundi 18 thamani ya fedha ikiwa Sh18 milioni.

Akizungumza leo Ijumaa Novemba 12,2021 katika hafla fupi ya utoaji mikopo hiyo, Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Tabora, Tumaini Mgaya amesema kwa sasa wanatoa mikopo yenye thamani ya Sh273.5 milioni.

Amesema fedha hizo zinatolewa kwa vikundi 54, wanawake wakipata Sh187 milioni kwa vikundi 38, vijana wakipata Sh80 milioni kwa vikundi vinane na watu wenye ulemavu Sh6.5milioni kwa vikundi 8.

Hata hivyo, Mgaya amesema idara yake imepokea Sh117.6 milioni ambazo ni robo ya kwanza ya asilimia 10 ya mapato ya ndani, ambapo Sh463 milioni zimetengwa kwa mwaka huu wa fedha.

Meya wa Manispaa ya Tabora, Ramadhan Kapela amevitaka vikundi vya vijana kuiga wanawake katika urejeshwaji wa mikopo.

Ameiagiza idara ya Maendeleo ya Jamii kuvichukulia hatua vikundi ambavyo vineshindwa kurejesha mikopo kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuvifikisha mahakamani.

"Vikundi vya akinamama na watu wenye ulemavu vinafanya vizuri katika ulkurejesha mikopo,Sasa na vijana waige kwao ili wengi zaidi wapate mikopo," amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Dk Yahaya Nawanda, amevitaka vikundi vikivyopewa mikopo kuthamini jitihada za Serikali katika kuwaona wanapata Mikopo itakayowanufaisha.

Chanzo: mwananchidigital